Kwa mujibu wa kitengo cha tarjama cha Shirika la Habari la Hawza, hatua za ukandamizaji za ukoo wa Aal Khalifa tangia vita vya Ramadhani hadi sasa dhidi ya Mashia wa Bahrain zimeongezeka kwa kiwango kikubwa. Kukamatwa na kuteswa kwa wananchi wa Bahrain pamoja na kufukuzwa na kuvuliwa uraia kwa makumi ya Wabahrain ni miongoni mwa hatua za ukandamizaji zinazofanywa na utawala wa kidikteta wa Aal Khalifa, vikosi vya usalama vya utawala wa Aal Khalifa vilivamia kwa njia ya kinyama nyumba za wanazuoni wa Kishia katika maeneo mbalimbali ya Bahrain na kuwakamata maulamaa na wanazuoni wa dini.
Katika muktadha huo, Jumuiya ya Al-Amal Al-Islami ya Bahrain imetoa taarifa na kuwaomba wananchi wote wa Bahrain waliomo ndani na nje ya nchi kuonesha hasira zao za wazi dhidi ya hatua hiyo ya kinyama ya Aal Khalifa kupitia harakati za amani.
بسم الله الرحمن الرحیم
﴿وَسَیَعْلَمُ الَّذِینَ ظَلَمُوا أَیَّ مُنقَلَبٍ یَنقَلِبُونَ﴾
صدق الله العلی العظیم
Jumuiya ya Al-Amal Al-Islami inalaani kwa maneno makali kabisa ya hasira na chuki shambulio la kipolisi la kigaidi na la kinyama lililofanywa na mamluki wa serikali ya Aal Khalifa dhidi ya nyumba za wananchi waumini wa Bahrain. Katika shambulio hili la kinyama, idadi kubwa ya wanazuoni wakubwa wa dini, shakhsia maarufu za kijamii pamoja na watoto wa Ayatullah Sheikh Isa Ahmad Qassim (Mwenyezi Mungu amhifadhi), walilengwa katika mwenendo hatari wa kulipiza kisasi unaodhihirisha hali ya kufilisika kisiasa na kimaadili ya serikali hiyo.
Taarifa iliyotolewa na Wizara ya Mambo ya Ndani, iliyojumuisha tuhuma na uongo wa batili kuhusu mawasiliano na uhusiano na Sepah na Wilayat al-Faqih ambayo ni fikra ya itikadi, si ruhusa ya kuwafanyia uvamizi wananchi waumini. Hatua hizi zote si chochote isipokuwa ni juhudi za kukata tamaa za kuhalalisha ukandamizaji wa kinyama na kulenga madhehebu ya Kishia pamoja na viongozi wa kidini na kitaifa; ukandamizaji ambao umeendelea kwa mfululizo na unajumuisha kutengwa pembeni, kufukuzwa na kuchochea fitna za kimadhehebu zilizopangwa ambazo serikali imekuwa ikizifuatilia kwa miaka mingi.
Jumuiya ya Al-Amal Al-Islami ya Bahrain inasisitiza kwamba; madai haya ya kawaida na yaliyokataliwa hayawezi kuwashinikiza wananchi wa Bahrain. Kuingiza majina ya wanazuoni na viongozi wa dini katika kampeni za kuvunja heshima na kuharibu taswira yao kupitia vyombo vya habari na usalama ni ishara ya wazi ya kuvamiwa kwa heshima ya watoto wa Bahrain, itikadi zao za kidini na kuchochea hisia za mamilioni ya watu huru ndani na nje ya Bahrain.
Kwa hakika, serikali ya Aal Khalifa kupitia kuvamia nyumba, kuwatisha wanawake na watoto, kuwakamata wanazuoni na vijana, pamoja na kuendelea na sera ya kuhalalisha mahusiano, ukandamizaji, kuvua uraia, kuwafukuza na kuwatesa wananchi, katika juhudi iliyoshindwa ya kuvunja irada ya wananchi na kuwafanya wapige magoti kwenye nguvu za kiusalama, imevuka mipaka yote mekundu.
Jumuiya ya Al-Amal Al-Islami inaibebesha serikali ya Aal Khalifa jukumu kamili la madhara ya ongezeko hili hatari la mvutano, na inaonya kuhusu kuendelea kwa njia hii ya kiusalama na ya umwagaji damu ambayo haitakuwa na matokeo isipokuwa kuongeza hasira za kitaifa na kusababisha mlipuko pamoja na kuanguka kwa serikali ya dhulma na madhalimu.
Kama walivyofukuzwa wakoloni hapo zamani, walinzi na wahifadhi wa Marekani na Wazayuni pia watafukuzwa, na Bahrain ni ya waumini, Waislamu na watu huru, wala hakuna nafasi kwa mamluki, wanafiki wa maslahi na wengineo.
Jumuiya ya Al-Amal Al-Islami inawataka wananchi wote watukufu wa Bahrain kuonesha hasira za wazi za kitaifa katika maeneo yote ya Bahrain, na inataka kuongezwa kwa harakati za kitaifa za amani kwa ajili ya kupinga dhulma na udikteta, pamoja na kutangaza mshikamano kamili na wafungwa na familia zao hadi pale watakapoachiwa wote mara moja na mashambulizi ya ukandamizaji pamoja na kulengwa kwa misingi ya kimadhehebu kusitishwa.
Aidha, Jumuiya ya Al-Amal Al-Islami inatoa wito kwa mashirika ya kimataifa ya haki za binadamu, Umoja wa Mataifa na dunia nzima kuvunja ukimya wao wa kuaibisha mbele ya jinai na uvamizi unaofanywa dhidi ya wananchi wa Bahrain, wanazuoni na shakhsia mashuhuri za kidini.
Wananchi wa Bahrain, kwa uimara na msimamo wao mbele ya ukandamizaji na ujeuri, huku wakishikamana na haki zao za kisheria, heshima na utambulisho wao, wataendelea kusimama kidete hadi kuanguka kwa dhulma na kupatikana kwa uhuru na uadilifu.
Maoni yako